Total Pageviews

Wednesday, August 24, 2011

Jinsi ya kuchagua mpiga picha, vitu 10 vya kuzingatia


Jinsi ya kuchagua mpiga picha, vitu 10 vya kuzingatia
Ndio siku yako kubwa, pamoja na mambo mengine yote yanayoendelea, unataka siku ya mwisho uwe na kumbukumbu bora ya siku hiyo, hapa ninamaanisha picha za mnato na picha za video. Ni kwasababuu hiyo basi kwamba ni muhimu ukachagua mpiga picha na kemera man wazuri ambao watakutendea haki na kazi yako. Na pengine hujui ni jinsi gani utabaini mpiga picha na kemera man wa kaliba hiyo, na hapa chini ndio natoa dokezo.
Kupiga picha za mnato na zile zinazotembea ni taaluma mbili zinazorandana ila hapa nitaongelea uchaguzi wa mpiga picha za mnato. Cha muhimu unataka matukio muhimu katika harusi yako yakamatwe barabara, zingatia:

1.       Umependezwa na kazi za awali za huyu mtu?
Kabla hata hujaanza kumfikiria huyo mpiga picha, hakikisha umeona kazi zake alizofanya awali, yaani wanakamati wanaweza kupendekeza watu kadhaa, sio mara zote huwa ni kutokana na ubora wa kazi za hao watu, saa nyingine huwa ni…kwahiyo sisitiza kukutana nao wakiwa na kazi zao, mara nyingi wapiga picha bora watakua na album ambazo wameweka kazi zao bora zaidi.

Je unaridhishwa na ubora wa kazi yake? Picha zake zinamvuto kwako? Mwanga na rangi katika picha zinavutia? Je style yake ndio unayoifikiria kwa picha zako? Kuna aina Fulani mahususi ya picha unataka na je ana uwezo wa kupiga picha za aina hiyo? (Maharusi wengi huenda kwenye professional houses kupiga picha hizi). Usiridhike na mmoja jaribu kuangalia kazi mbili tatu, kama hujaridhishwa basi hamna haja ya kumfikiria zaidi.

Sasa basi, kuna mtindo, hasa kama mpiga picha anatokea kwenye studio au kampuni, ukaongea na mtu mwingine au ukaoneshwa picha za mpiga picha mwingine ila siku ya siku ukaletewa mtu mwingine. Onesha tangu mwanzo kwamba hautaentertain ujinga huo, kuwa mjanja kufahamu jina la mpiga picha tangu mwanzo na kusisitiza kuwa ndiye utakayemtegemea siku hiyo, fanya malipo ya awali na kubali kutoa malipo ya mwisho mara tu baada ya kupokea kazi yako na kuridhishwa nayo.

2.       Ana uzoefu wa kiasi gani?
Kama nyongeza ya hapo juu, huyu mpiga picha ana uzoefu wa kiasi gani katika upigaji picha za harusi na shughuli kama hizo? Uzoefu unasaidia kwani mpiga picha huyu ana uwezo wa kujua au kuotea ni matendo gani yatatokea, wakati gani yatatokea na hivyo kuwa tayari kuyakamata, mgeni katika upigaji picha wa shighuli hizi ataishia kukimbia kimbia kufuata matukio anaposikia labda MC kasema kitu na kuyakosa yote kwa kutokua positioned at the right place at the right time.

Mimi ni mmoja wa wale wanaochallege kutopata kazi kutokana na ukosefu wa experience, sasa bila kupewa kazi hiyo experience itatoka wapi? Kama umependezwa na kazi za mpiga picha ambaye bado hajapata uzoefu wa kutosha na shughuli hizi, unaweza kumsaidia kwa kumpatia orodha ya matukio muhimu ambayo wewe unataka yakamatwe, mtiririko wa matukio katika siku hiyo na sitting arrangement ya wageni wako, kwa jinsi hii atakua tayari zaidi na kufanya kazi yake kwa ufanisi. Plus utakua umemuongeze uzoefu, good for you.

Uzuri mmoja wa kuwa na mtu mzoefu ni kwamba ukiacha mambo ya ratiba, anaweza kupredict and anticipate things that could wrong na anakua prepared kudeal navyo.

3.       Yuko tayari kutoa kemera ngapi?
Mpiga picha mmoja kusema kweli huwa hatoshi kucover event nzima peke yake, wapiga picha wajanja wenye kujua kazi yao huja na team ya watu kadhaa, kamera walau mbili au tatu kutokana na ukubwa wa sherehe, na wengine wanakua ni technical guys, taa, stands na vitu kama hivyo. Je mpiga picha wako ana timu yake? Huyu ni Yule ambaye umemchuja katika awamu hizo mbili hapo juu, so hao kemera man wengine watakua ni jukumu lake kuhakikisha ubora aliokuahidi. Itabidi tu uassume kwamba kazi nzuri ulizoona kwa album ni matokeo ya yeam work hiyo hiyo atakayokuahidi. Usijidanganye ati atafanya kazi yote mwenyewe. Kama ndio hivyo huu ndio muda wa kumdrop huyu hata kama amefaulu hatua nyingine.

4.       Anafanya kazi na Mpiga picha za video?
Mara nyingine hawa watu wawili huwanya kazi kama team pia, je mpiga picha wako anafanya kazi na mpiga picha za kutembea (moving picture), hii itakua vema kwako kwani ukipata package hii inamaanisha savings on your side, lazima ilete maana, kama ukipata video man mwingine na gharama zao pamoja zikawa pungufu zaidi then kuwa huru kutafuta video man mwingine. Inabidi uwe makini usije uakasettle for this deal wakati video man ni bogus, makala nyingine itaeleza jinsi ya kuchagua video man.

5.       Wanaweza kufanya kazi pamoja?
Kama anafanya kazi solo je ana uwezo wa kufanya kazi na video man mwingine? Yani wakafanya kazi kwa kushirikiana, usije ukaishia kuwa na mataa kumi, tano za video man tano za kamera man mpaka wakakuharibia ambiance ya siku yako, nyaya zinapishana kila mahali. So hakikisha kuwa hawa wawili hata kama hawafahamiani watakua tayari kukaa pamoja na kuplan jinsi watakavyofanya kazi pamoja.

6.       Je ni kazi yake mahususi au ni part time job?
Mpiga picha wako hii ndio kazi yake mahususi inayomuweka mjini au ni hobbie tu, a part time thing to make extra money on the side? Hobbies, watu wengine wanachukulia hobbies zao na part time jobs very seriously na inawezekana isiwe tatizo, lakini uzoefu unaonesha kuwa watu huwa hawako serious na part time things, atakisogeza mpaka atakapoweza, kikwazo kidogo kikitokea haoni shida kuingia mitini na pesa na kazi yako. Nimepata hii experience first hand so sitanii. Make sure unafanya kazi na mtu serious, ideally iwe kampuni au studio na sio individual, wanaweza kuwa matapeli.

7.       Tabia yake je? Much know sana au anasikiliza mteja wake anataka nini?
Uzoefu unapoingia kichwani, unajaribu kumueleza mpiga picha idea zako kwasababu kuna vitu mahususi ungependa ambavyo sio vya kila siku nay eye anakwambia, “usijali niachie kila kitu, najua, najua si unataka wakati mnaingia….najua usijali” mmmh ujue huyo ameshakremu picha za kupiga, na ukija kuangalia album yako nay a kina Kiwanga ni the same pictures different people!! Unless huna makuu ukaamua kumuachia mpiga picha afanye kazi yake the best way anavyoijua, hakikisha mpiga picha wako anauwezo wa kucommunicate na kusikiliza matakwa yako na ayaelewe.

Kama ni Yule ambaye sio mzoefu na unafikiria kumpa chance, drop him now, kwasababu utamuelekeza na kumpa nyenzo zote za kumsaidia na yeye ataishia kufanya anachojua yeye, why? Hajasikia kitu chochote ulichosema, labda hata haelewi kuwa kupata hiyo kazi ukichukulia ukosefu wake wa uzoefu ni bahati, atakuharibia kazi yako!!

8.       Vifaa vya kazi na teknologia
Nitakubali kuwa mimi sio mtaalamu wa kamera na wasomaji wangu wengi vilevile, lakini ni vizuri kuhoji uwezo wa vifaa vya mpiga picha wako, anaweza kutoa picha nzuri usiku, mchana, kwa mbali karibu? Lakini walau awe na kamera yenye uwezo unaokubalika (will research some more) na vifaa vingine kama taa na milingoti yake.

Muhimu sana awe na packup set ya vifaa vyake in case anything goes wrong, wazoefu utaweza kuwatofautisha hapa kwasababu kwa wao huu ndio utaratibu wa kazi, feki watakua na kamera za kuazima bila backup ya aina yoyote.

9.       Kukabidhi kazi
Kazi ya picha mara nyingi huwa tayari hata siku inayofuata kama zitaenda studio moja kwa moja, hata hivyo wiki moja ni muda wa kutosha kwa mpiga picha wako kuwasilisha kazi yako. Ana uwezo huo? Mkubaliana kazi itakua tayari baada ya muda gani.

Kazi itawasilishwa katika media ipi? Hard copies ndani ya album? Bila album? Na CD au la? Picha ngapi, size gani? Album ngapi? Lazima mkubaliane ili kusiwe na lawama mwisho wa siku.

10.   Je unapata Value for your money?
Hiki ni kitu muhimu sana ambacho watu wengi huwa kinawapita bila wao kujua. Kuna wapiga picha wanauza majina, in which case wanakupumbaza na wewe unafeel chochote watachosema lazima ndio chenyewe. Sio kweli siku zote, mara nyingi wapiga picha wenye majina huwa wako in demand sana na huwa wanashawishika kuchukua kazi nyingi kwa wakati mmoja, hawachelewi kukuahidi kila kitu and then siku ya siku wanakutumia mtu baki, utafanya nini? Siku ndio imeshafika, umeshatumia muda wako mwingi kumake sure things go right ghafla kitu kama hiki kinatokea.

Niamini nitakapokuambia kuwa kuna wapiga picha bora sana ambao hawana majina, na ukifuata hizi hatua utaweza kuwagundua baadhi. Hawa watakua na gharama nafuu lakini watakufanyia kazi ambayo otherwise ungelipa mapesa na mapesa kwasababu tu ya jina.

Basically kama mpiga picha amepasi hizo hatua hapo juu then ataweza kukufanyia kazi itakayokuridhisha, hata kama gharama yake haitakua nafuu kihivyo, atakua muadilifu na muaminifu, so make sure you get value for you money, quality and peace of mind is what you want so you can relax on your day.

Sio muhimu sana lakini bonus kama mpiga picha huyu na timu yake watavaa nadhifu siku hiyo, sio mbaya kutinga suti hivi so akablend na wageni.

Mwisho nasemaje, tujenge tabia ya kuwa tunasign mikataba na hawa watu, wengi wanataka malipo yote up front, au nusu ya kumbook, nusu siku ya harusi shughuli inapoanza, akiharibu kazi au asipokuridhisha ni wachache wenye ustaarabu wa kusema wakurefund pesa zako kwa kuwa wameshindwa kudeliver as expected, wengi watakuyeyusha utabaki unasononeka with nothing to hold this guy against, huna picha au mbaya na pesa umelipa. Mikataba inabidi ieleze vema nini kinategemewa kustahili malipo, na kwasababu harusi ni siku isiyorudia, akiharibu kazi inabidi akulipe fidia, hii itawafanya wapiga picha kuwa makini zaidi katika kazi zao, au unasemaje? Nitawawekea templates za mikataba siku za usoni.

Tuesday, August 23, 2011

Hii ni Migowoods Stationery iko magomeni mapipa, karibuni sana!!!



 Pichani ni Chief Secretary wa Migowoods Mage

 Chief Secretary akiwa anaclick....


Ujasiriamali ndio neno jipya. Kila mtu anaongelea habari za ujasiriamali. Pengine hii inatokana na wengi wetu kutambua kwamba nyakati zimebadilika na ujasiriamali ndio njia iliyo sahihi zaidi kama mtu anatamani mafanikio ya kweli maishani.Vijana ndio chachu zaidi ya ujasiriamali au naweza kusema ndio wanategemewa zaidi kuendeleza ujasiriamali hususani katika ulimwengu wa leo wa sayansi na tekinolojia.
Pamoja na nia nzuri walizonazo vijana, pengine ukiwemo wewe unayesoma makala hii, kipo kizingiti ambacho ni lazima watu wajifunze mbinu mpya za kukivuka. Kizingiti hicho ni aina ya elimu itolewayo mashuleni. Kwa bahati mbaya elimu zitolewazo mashuleni bado hazijawekwa katika msingi unaomuwezesha kijana kujiajiri au kwa maneno mengine kuwa mjasiriamali pindi amalizapo masomo yake.

Bado tupo katika ule mfumo wa kikoloni. Ukimaliza shule unachotakiwa ni kuanza kutafuta kazi. Zunguka jijini Dar-es-salaam kwa mfano, utakutana na vijana wengi wasomi waliohitimu katika vyuo vikuu mbalimbali nchini wakiwa wamebeba vyeti vyao kwenye vijifuko vya plastiki wakizurura kusaka ajira. Hakuna anayefiria kujiajiri kwa kutumia elimu aliyoipata chuoni. Kwanini? Ndivyo ilivyo. Elimu aliyopewa haikumuandaa.Utakutana na engineer wa umeme ambaye hajawahi kubadilisha hata balbu!(nimeongeza chumvi kidogo hapa lakini kuna ukweli ndani yake!) Amesomea nadharia zaidi ya vitendo. Utakutana na mwanafunzi mhitimu wa masomo ya kilimo na mazingira ambaye hajui shamba ni nini.Hilo ni kosa katika mfumo wetu wa elimu. Ni lazima serikali ichukue jukumu la makusudi kubadili mfumo huo.

Lakini wapo wengine wengi ambao wana nia ya kweli ya kuwa wajasiriamali. Wana nia ya kujiajiri. Leo tutaangalia jinsi gani mjasiriamali chipukizi aanzishe kampeni yake. Si ushasikia kwamba biashara siku hizi ni kujuana? Ujasiriamali pia. Ni muhimu sana kujua ni nani au ni wapi uende endapo mambo yatakwama. Siongelei wapi uende kutoa au kupokea rushwa.La. Nataka kuongelea kitu kinachoitwa na wenzetu wa magharibi “networking”.Kwetu sisi hiki ndicho tunachoita “mtandao”.Mitandao ya kijamii kama vile facebook,twitter,myspace nk ni sehemu nzuri ya kutengeneza network.Itumie vizuri.

Ni muhimu kutengeneza mtandao mzuri kama unataka kuwa mjasiriamali makini na hususani kama unataka kufanikiwa. Kumbuka kwamba hapa hatuongelei kubadilishana business cards peke yake bali kumjua mtu kwa nia njema ya kusaidiana.Kumbuka neno ni “kusaidiana” na sio wewe pekee kupokea msaada.Lazima pawe na nia njema ya kusaidiana.

Kabla sijaanza kuorodhesha mbinu mbalimbali za kutengeneza ‘mtandao’ wako, naomba nikwambie kwamba siri ya kwanza ya kuanza kuwa mjasiriamali ni maandalizi.Jiandae kwa mtaji,elimu(ya darasani na mtaani),mbinu za kibiashara nk. Pili hakikisha kwamba una mapenzi ya dhati na hicho unachotaka kufanya.Usiingie kwenye biashara au ujasiriamali kwa sababu tu umemuona fulani amefanya hivyo.Kuna umuhimu mkubwa wa kujitambua katika suala zima la ujasiriamali. Baada ya kusema hivyo,sasa tuingie kwenye maeneo ya kutengeneza mtandao wako kama mjasiriamali;

  • Washindani wako: Biashara ni ushindani lakini sio uadui.Kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio ni vizuri sana ukawajua washindani wako wa kibiashara.Pata vipeperushi vyao,tembelea tovuti zao,wajue wateja wao na kwanini hao watu ni wateja wao.Kisha jitambulishe kwao.Najua hapa unasema;nijitambulishe?!! Ndio,jitambulishe.Kama nilivyosema ni washindani lakini sio maadui zako. Mshindani wako anaweza kukufaa pia.Anaweza kuzidiwa na kazi akakusukumia zingine.Jitambulishe,jenga uhusiano mzuri wa kibiashara.Isitoshe nyote mpo kwenye biashara moja,sekta moja.Ya kesho hamyajui.Kama kuna chama au ushirika wa watu waliomo kwenye eneo lako la ujasiriamali,jiunge.
  • Vyombo vya Habari: Siku hizi kuna aina nyingi zaidi za vyombo vya habari na mawasiliano. Kuna magazeti,televisheni,radio, blogs nk. Kama mjasiriamali,ni muhimu ukajuana na watu wanaoendesha au hata kumiliki vyombo hivi vya habari. Na zaidi angalia vile ambavyo vipo karibu zaidi na eneo lako la ujasiriamali.Ni rahisi zaidi kwa habari ya ujasiriamali wako kuandikwa gazetini,kuongelewa radioni,kuonekana kwenye televisheni nk kama watu wa vyombo vya habari wanajua unachofanya.Mara nyingi watu wengi wa habari wanapotaka kufanya utafiti wa jambo fulani huanza kwanza kwa kuangalia “sources” alizonazo. Kumbuka kwamba kuandikwa mara kwa mara juu ya kazi zako,ujasiriamali wako, husababisha watu kukukumbuka,kukuheshimu na hivyo kuwa rahisi kwao kufanya biashara na wewe.
  • Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO): Mjasiriamali makini ni yule ambaye anadhamiria kuisaidia jamii yake kwa njia moja au nyingine. Zipo faida mbalimbali za kibiashara kwa mjasiriamali ambaye hurudi nyuma na kusaidia jamii yake.Kuna faida za mapunguzo au unafuu fulani wa kodi(waulize TRA watakupa data zaidi).Isitoshe jamii iliyo bora,iwe kiafya,kielimu nk ni wateja wako wazuri wa siku za mbeleni.
    Hivyo ni muhimu kujuana na watu mbalimbali wanaoendesha mashirika yasiyo ya kiserikali ama NGOs.Dhamini shughuli zao mbalimbali.Ukifanya hivyo(mara nyingi ni bei rahisi zaidi) unakuwa umesaidia jamii yako na pia umetangaza biashara yako.Lakini kuwa makini. Zipo NGO kibao siku hizi.Nyingine ni mitaji ya watu.Achana nazo.Tafuta zile ambazo ni halali na kazi wanayofanya inaonekana katika jamii.
  • Mwanasheria mmoja au wawili: Kama ilivyo katika maeneo mengine,msaada wa kisheria unaweza ukahitajika wakati wowote katika ujasiriamali.Unaweza kutaka ushauri,unaweza kushitakiwa nk. Ni vizuri kama ukawa unajuana na watu mbalimbali waliopo kwenye uwanja wa wanasheria. Mara nyingi watu tunaelewa mambo vizuri tunapokuwa tunaongea na watu ambao tunafahamiana nao kwa njia moja au nyingine.Wazungu wanasema unakuwa “more comfortable”. Sasa kwa sababu huwezi jua ni lini utahitaji msaada wa kisheria, ni vizuri ukajuana na mwanasheria mmoja au wawili kwa minajili ya kukusaidia endapo utaalamu wao utahitajika.
    Kumbuka tu kwamba hapa siongelei msaada wa bure bali malipo fulani ingawa kutokana na kujuana huko,ni rahisi kupata punguzo la bei na pia ile faraja ya kuongea na mtu unayejuana naye.Wakati mwingine unaweza kumuuliza tu “rafiki mwanasheria” kuhusu hoja fulani ya kisheria wakati wa chakula cha mchana(lunch) na ukawa umepata jibu.Free.
  • Mwakilishi wako wa kisiasa: Bahati mbaya au nzuri ni kwamba hakuna biashara au ujasiriamali ambao unaweza kujitenga moja kwa moja na siasa za nchi au eneo fulani. Kuanzia kwenye ugawaji wa maeneo ya biashara, utolewaji wa leseni za biashara,sera mbalimbali za biashara nk lazima kuna ‘siasa’ fulani. Sasa kwa sababu sera hizo huwa zina mkono wa siasa,ni muhimu sana kujuana na wahusika au watungaji wa sera hizo ambao mara nyingi ni wanasiasa.Ukiwajua au kujuana na wanasiasa wa eneo lako,ni rahisi kwako wewe kufikisha ujumbe,malalamiko yako na pia hisia zako katika mambo mbalimbali.Kumbuka kwamba biashara au ujasiriamali wako ni sehemu ya jamii.Ni muhimu ukamjua Balozi,Mjumbe,Mbunge,Waziri nk kutoka katika jumuiya yako au mahali ilipo biashara yako.Usije kujidanganya kwa kusema ‘ah mimi sitaki kabisa kujuana na wanasiasa”.Utakuwa unakosea na utakuwa sio mjasiriamali makini.
Kwa ufupi hayo ni maeneo ambayo ni muhimu kuyazingatia endapo “ujasiriamali” ni kitu ambacho unakitamani au tayari unakifanya. Lakini kama ambavyo nimekuwa nikisisitiza katika makala zangu; fanya kazi kwa bidii na maarifa. Hiyo ndio siri ya msingi ya mafanikio katika maisha. Kujuana na watu mbalimbali muhimu peke yake haitoshi. Kazi mbele. Tukutane tena next time....

Monday, August 22, 2011

Monday, August 15, 2011

Wakurugenzi walipohitimu... Rhhaaaaaa!!!!

 Wadau wa Migowoods Warda Juma na Sadique Bwanga
 Wadau wengine wa migowoods kutoka kushoto kuelekea kulia wa kwanza ni Njugu Zahoro, Hamza Abeid, Omari Yusuph, Warda Juma, na Kaka mkubwa Khatibu Mohamedi, wakiwa wanawapa kampani wakurugenzi wetu walipohitimu chuo, katika viwanja vya kareem jee
 Warda Juma na Sadique Bwanga Kwenye mahafali yao

Hii nayo ni miongoni mwa Harusi zilizoshuhudiwa na Migowoods Productions...

 Mdau wa Migowoods Bw. Omar Yusuph akiwa sambamba na Bi harusi siku ya tukio, ilikuwa magomeni mapipa
 Wakitoka ndani kuelekea nje kwenye kiamu....
 wakiwa nje katika pozi la pamoja...
 maulidi yalifana sana kwa kweli...
Hapo sasa......

Sio Filamu tu, sisi tunapiga picha za matukio yote hii ni moja ya harusi tuliyofanya...

 Kaka mkubwa wa migowoods akipeana mikono na maharusi Bw. Amir na Bi Aziza.... ilikuwa ilala Amana hiyo
 Cameraman wetu Bw. Mtumwa Bilal akiwa kazini kuhakikisha hapitwi na tukio lolote.
Maharusi wetu wa siku hiyo Bw. Amir na Bi. Aziza wakiwa wamepakatana. Inshaallah mola awadumishieni Upendo

Wadau wa Migowoods hao....

 Bwana Amon Ntevi wa Migowoods akiwa sambamba na Mkurugenzi Mtendaji Sadique Bwanga ndani ya Htl ya Kempinski...
Mkurugenzi mtendaji wa Migowoods Productions katika pozi la picha ndani ya Kempinski....

Mambo ya Kempinski hayoo......

Bwana Sadique Bwanga wa Migowoods Productions akiwa sambamba na mdau wetu mwengine Bwana Gideon Ntevi katika htl ya Kempinski wakifatilia mkutano wa wauza mafuta ya ufuta kutoka Maleysia...

Mambo ya ndoa hayo...

BWANA SADIQUE BWANGA (kulia) AKIWA NA SWAHIBA WAKE WA SEKONDARI BWANA AJMAR AMIR SIKU YA NDOA YAKE HUKOOO VINGUNGUTI.

Mambo ya Uzinduzi wa Big Brother Amplified Hayo ndani ya Nyumbani















Maandalizi ya Filamu yetu ya kwanza tukiwa kama MIGOWOODS PRODUCTIONS